Nyumbani

Thursday, August 15, 2013

YOU ARE MY DESTINY.

PEKE YANGU SITOWEZA, BILA WEWE MUHISANI
HAKIKA WANIPENDEZA, HABIBY YAH NURULAINI.
WEWE WANGU MUUJIZA, UNA NIJAZA AMANI.
UNA NIONDOA KIZA, NA TONGO TONGO ZA MBONI.
 NAJITUPA NAJILAZA, NIKUMBATE MAUNGONI
JAPO KWANGU SI WA KWANZA, YOU ARE MY DESTINY.

Tuesday, April 17, 2012

CHUNGENI AFYA ZENU

MWENDA TEZI NA OMO MAREJEO NI NGAMANI.
MWENYE KUPENDA KWA MACHO YE HAISHI KUTAMANI
MWENYE DHATI  NA MAHABA HABAINIKI MACHONI.
CHUNGENI AFYA ZENU NGONO ZEMBE EPUKENI.

Monday, March 26, 2012

MOYO WANGU NI MCHANGA

PENZI HUJENGWA NA VINGI INGAWAJE SIVIONI,
TABASAMU TU HALITOSHI KUCHEKEANA USONI,
HISIA ZANGU ZA NDANI ZINAISHIA KIFUANI,
MOYO WANGU NI MCHANGA KUJIINGIZA PENZINI.

TUTOE HUMU GIZANI

NCHI YANGU INAUMWA NA UCHUMI TAABANI.
UNAPANDA NA KUSHUKA KAMA BEI MNADANI.
PESA HAICHENJIKI ELFU KUMI KITU GANI.
UKABILA NI KIINI KUAJIRIWA KAZINI.
DINI IPO CHINICHINI HAISEMWI HADHARANI.
PESA YAKO BEI GANI UKAE MADARAKANI.
UWEZO WA KAZI GANI TOA PESA MFUKONI.
AJIRA OTA NDOTONI WEWE NDUGU YAKO NANI.
SIASA JANJA YA NYANI UFISADI NDIO FANI.
EEH MOLA WETU MANANI TUTOE HUMU GIZANI.

MACHO YAKE YANASEMA

MACHO YAKE YANASEMA, HAKIKA NI MWENYE HUBA.
NA AMESHINDWA KUSEMA, MOYONI YANAMKABA.
TENA YEYE MTU MWEMA,MWINGI WA NYINGI NASABA.
USIKU HAUNA WEMA, ANALALA SAA SABA.
NA HAISHI KUKUSEMA, KWENYE NDOTO KWA MAHABA.
KESHO SEMA NAE VYEMA,MPUNGUZIE SHULUBA.

NYODO KAMA VIFUNGO

MACHO YAKO YENYE WANJA NAYO NDEFU YAKO SHINGO.
UMBO LAKO NANE NAMBA NA HUO MWENDO  MARINGO.
SAUTI KAMA KASUKU NA NYODO KAMA VIFUNGO.
AMINI MI NAKUPENDA DHAMBI KUSEMA UONGO

MFANO KAMA HARIRI

WANGU KIPENZI MZURI, MFANO KAMA HARIRI.
WEWE KWANGU NI HABARI, KIFANI CHAKO DINARI.
ZIPITE ENZI DAHARI, UBAKI WANGU UTURI.
MOLA AKUJAZE KHERI, AKUEPUSHE NA SHARI.