MWENDA TEZI NA OMO MAREJEO NI NGAMANI. MWENYE KUPENDA KWA MACHO YE HAISHI KUTAMANI MWENYE DHATI NA MAHABA HABAINIKI
MACHONI. CHUNGENI AFYA ZENU NGONO ZEMBE EPUKENI.
NCHI YANGU INAUMWA NA UCHUMI TAABANI. UNAPANDA NA KUSHUKA KAMA BEI MNADANI. PESA HAICHENJIKI ELFU KUMI KITU GANI. UKABILA NI KIINI KUAJIRIWA KAZINI. DINI IPO CHINICHINI HAISEMWI HADHARANI. PESA YAKO BEI GANI UKAE MADARAKANI. UWEZO WA KAZI GANI TOA PESA MFUKONI. AJIRA OTA NDOTONI WEWE NDUGU YAKO NANI. SIASA JANJA YA NYANI UFISADI NDIO FANI. EEH MOLA WETU MANANI TUTOE HUMU GIZANI.
MACHO YAKE YANASEMA, HAKIKA NI MWENYE HUBA. NA AMESHINDWA KUSEMA, MOYONI YANAMKABA. TENA YEYE MTU MWEMA,MWINGI WA NYINGI NASABA. USIKU HAUNA WEMA, ANALALA SAA SABA. NA HAISHI KUKUSEMA, KWENYE NDOTO KWA MAHABA. KESHO SEMA NAE VYEMA,MPUNGUZIE SHULUBA.
MACHO YAKO YENYE WANJA NAYO NDEFU YAKO
SHINGO. UMBO LAKO NANE NAMBA NA HUO MWENDO
MARINGO. SAUTI KAMA KASUKU NA NYODO KAMA VIFUNGO. AMINI MI NAKUPENDA DHAMBI KUSEMA UONGO
MSHUKURU MOLA WAKO KUFIKA MWISHO WA MWAKA. JUA SI UJANJA WAKO BALI
YEYE ALITAKA. MTUKUZE MUNGU WAKO NENDA KATOE SADAKA. MBILI NA KUMI NA TATU UWE MWAKA WA BARAKA. NAKUTAKIA NAFAKA NA PIA KHERI YA MWAKA.
KWAKO NIMEPATA PENZI MOTO ZAIDI YA JUA. KAZI ZA NJE SIZITAKI NAOGOPA KUUGUA. KWAKO TULI NIMERIDHI WENGINE WOTE PANGUA. DAIMA DAWAMU NAWE ZIJE MVUA NA JUA
MGOMBA WANIPA SHAKA NI MTI AU NI UA. NA TENA UNATUMIKA SHEREHE KUZIPAMBIA. UKIZAA NAUKATA NA HAUWEZI KUKUA. KAMA UNGEKUWA MTI TANURI NINGECHIMBIA. ILI NICHOME MKAA UCHUMI KUJIKWAMUA. WALA HAUNA MATAWI NIWEZE KUNING'INIA. MBONA NDIZI UNAZAA KAMA MGOMBA NI UA. TENA BILA YA MSIMU TUNDA UNAJIZALIA. HAKIKA WANITATIZA MASWALI KUNIJAZIA. WAUNGWANA NIJUZENI MAJIBU KUNIPATIA. ETI MGOMBA NI MTI AU MGOMBA NI UA?
KITAMBI KIMENIPONZA,SINA HAMU ASILANI. KIMENIFANYA NAWAZA MAISHA SI YA
THAMANI. MAHARI MARA YA KWANZA
NATAKIWA MILIONI. WAKASHINDWA KUNIOZA KWA LAKI TANO JAMANI. NIKAMPENDA SHARIZA ASILI YA ARABUNI. ILE TU KUMPOSA DHAHABU ZA MILIONI. NI KITAMBI SINA PESA MI KABWELA KAMA NINI. KITAMBI KINANIPONZA NAKOSA MKE JAMANI.
ZILE SUNGURA NA FISI, HADITHI NILISHAACHA. TENA KWANGU NI NAJISI, NA NDOTO ZA ALNACHA. MAPENZI YA YANGU NAFSI, KWAKO SIWEZI KUFICHA. SIPOKUONA NAJIHISI,KIDOLE BILA YA KUCHA. PENDO LAKO MAKHUSUSI,NI MWANGA KILA KUKICHA.
PEKEE NI ABADANI, SITOWEZA ASILANI. BILA WANGU MUHISANI, WA
KUNIENZI NYONDANI. KETI ZA KIBARAZANI, BARIZI ZA UPENUNI. LISHE NIWAPO JANGWANI, BAKIA BAKI MWANDANI.