Nyumbani

Monday, March 26, 2012

MGOMBA NI MTI AU UA?

MGOMBA WANIPA SHAKA NI MTI AU NI UA.
NA TENA UNATUMIKA SHEREHE KUZIPAMBIA.
UKIZAA NAUKATA NA HAUWEZI KUKUA.
KAMA UNGEKUWA MTI TANURI NINGECHIMBIA.
ILI NICHOME MKAA UCHUMI KUJIKWAMUA.
WALA HAUNA MATAWI NIWEZE KUNING'INIA.
MBONA NDIZI UNAZAA KAMA MGOMBA NI UA.
TENA BILA YA MSIMU TUNDA UNAJIZALIA.
HAKIKA WANITATIZA MASWALI KUNIJAZIA.
WAUNGWANA NIJUZENI MAJIBU KUNIPATIA.
ETI MGOMBA NI MTI AU MGOMBA NI UA?

No comments:

Post a Comment